Simba SC warejea kambini

WACHEZAJI wa Simba SC wamerejea kambini kwa maandalizi kwa ajili ya mechi za NBC Premier League na CRDB Federation Cup.

Katika msimamo Simba SC ipo nafasi ya pili imekusanya pointi 58 baada ya mechi 25 tofauti ya pointi 2 na vinara wa ligi ambao ni Yanga SC wenye pointi 60.

Mchezo uliopita Simba SC ilipata ushindi wa goli 1-0 Dodoma Jiji FC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex. Mchezo ujao kwenye ligi ni dhidi ya Pamba Jiji FC, unatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2026 Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mzunguko wa pili.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema baada ya mapumziko mafupi wachezaji wanarejea kambini kwa maandalizi ya mechi zijazo.

“Baada ya mapumziko wachezaji wanarejea kambini kwa maandalizi ya mechi zinazofuata malengo ni kuona tunaendelea kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ushindani,”.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.