Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemteua Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za Tanzania zinazoshiriki mpira wa miguu.
Makonda ametangaza uteuzi huo leo Mei 28, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, Haji Manara atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo jukumu lake kubwa litakuwa kuzungumzia na kuratibu mawasiliano ya timu zote za Taifa upande wa mpira wa miguu.
Makonda amesema uteuzi huo ni sehemu ya jitihada za kuongeza nguvu katika mawasiliano, masoko pamoja na taswira ya timu za Taifa ndani na nje ya nchi.
Haji Manara ni mmoja wa watu maarufu katika masuala ya mawasiliano ya michezo nchini Tanzania, akiwa amewahi kufanya kazi na klabu mbalimbali kubwa za soka nchini.
Uteuzi huo umeanza kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka na wadau wa michezo nchini huku wengi wakisubiri kuona mchango wake katika kuimarisha mawasiliano ya timu za Taifa.
BARUA 25 za RAIS! AFICHUA KUFIKA HADI kwa PAPA LEO – “TUMEDANGANYWA TAARIFA SIYO ALIZOANDIKA RAIS”..