Ubabe Mtupu! Yanga SC Yatinga Nusu Fainali Bila Huruma Kombe la Muungano

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano 2026 baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Muembe Makumbi City katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Yanga walionesha ubora wao mapema katika mchezo huo, wakitawala kabisa dhidi ya wapinzani wao na kupata bao la kwanza dakika ya 17 kupitia Prince Dube akimalizia pasi safi kutoka kwa Stephane Aziz Ki (Okello).

Dakika 34, Frank Assinki aliongeza bao la pili kwa kichwa baada ya mpira wa krosi kutoka kwa Shekhan Khamis, kabla ya Shekhan mwenyewe kufunga bao la tatu dakika ya 38 kwa shuti kali lililomshinda kipa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama cha kwanza, ambapo Prince Dube alikamilisha ushindi wa Yanga kwa bao lake la pili dakika ya 57, akimalizia pasi safi kutoka kwa Edmund.

Ushindi huo unaendeleza ubabe wa Yanga SC kwenye mashindano ya ndani na kuwapandisha hatua ya nusu fainali wakiwa na morali kubwa kuelekea hatua zinazofuata za Kombe la Muungano.

FT: Yanga SC 4-0 Muembe Makumbi City
⚽ 17’ Prince Dube (🅰️ Okello)
⚽ 34’ Frank Assinki (🅰️ Shekhan)
⚽ 38’ Shekhan Khamis
⚽ 57’ Prince Dube (🅰️ Edmund)