Fountain Gate vs Simba SC kupigwa leo Aprili 15, 2025 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu.
Aboubakar Ally kocha wa Fountain Gate amesema kuwa wametoka kucheza mchezo wa CRDB Federation Cup dhidi ya Azam FC hivyo wamejiandaa kuwakabili wapinzani wao.
“Tumejiandaa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba SC, tumekuwa na muda wa kuzungumza kwa kuwa tunahitaji kuwatengeneza zaidi wachezaji wetu kuelekea mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
“Kila mchezaji anatambua kwamba ni mpinzani wa aina gani ambaye tunakutana naye hivyo tupo tayari kuwakabili wapinzani wetu na aina ya mechi ambayo tunacheza tutatumia mbinu zote kupata matokeo hasa kwa kutumia nafasi ambazo tutapata,”.
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.
“Tunatambua aina ya upinzani ambao tutaupata lakini tumefanya maandalizi mazuri na malengo ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu,”.
Kwenye msimamo Founatin Gate ipo nafasi 14 ikiwa na pointi 16 baada ya mechi 17 inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 36 baada ya mechi 17.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.