Yanga SC 1-0 TMA Stars CRDB Federatin Cup ni matokeo ya mchezo wa leo hatua ya 16 bora ambao umechezwa Uwanja wa KMC Complex.
Goli la ushindi la Yanga SC limefungwa na kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli dakika ya 69 ya mchezo.
Ni wazi kuwa Yanga SC ni mabingwa watetezi wa taji hilo hivyo wanaendelea safari kupambania taji lao ambalo lipo mkononi mwao.
Katika dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote ambapo ubao ulisoma Yanga SC 0-0 TMA Stars.
Ushindi huo ni rekodi nyingine kwa Yanga SC kuendelea kucheza mechi kwa msimu wa 2025/26 kwa mashindano ya ndani bila kupoteza.
Kwenye ligi ni mechi 18 mfululizo imecheza msimu wa 2025/26 bila kupoteza ikiwa inashikilia namba moja kwenye msimamo wa NBC Premier League.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.
Curacao's players pose for a team photo before the start of the World Cup qualifier football match between Jamaica and Curacao at the National Stadium in Kingston, Jamaica on November 18, 2025. (Photo by Ricardo Makyn / AFP) (Photo by RICARDO MAKYN/AFP via Getty Images)