Pamba Jiji FC vs Yanga SC kituo kinachofuata

Pamba Jiji FC vs Yanga SC kituo kinachofuata katika NBC Premier League 2025/26 kwa wababe hawa wawili kusaka pointi 3 muhimu.

Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons ni matokeo yaliyopita kwenye mchezo wa ligi na mchezaji bora alichaguliwa Allen Okello raia wa Uganda ilikuwa ni Aprili 4, 2026, Uwanja wa KMC Complex.

Mashujaa FC 0-0 Pamba Jiji FC matokeo yaliyopita kwa wababe hawa mchezo uliochezwa Aprili 4, 2026 Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wareli Kigoma.

Katika mchezo huo mlinda mlango namba moja wa Pamba Jiji FC, Yona Amos alitwaa tuzo ya mchezaji bora.

Wababe hawa wawili wanatarajiwa kukutana Uwanja wa CCM Kirumba kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Wenyeji Pamba Jiji FC nafasi ya 5 kwenye msimamo pointi 26 huku Yanga SC ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 41 kwenye msimamo uliofanyiwa maboresho hivi punde.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.