Simba SC: Mpanzu bado ana mkataba

UONGOZI wa Simba SC umebainisha kuwa mchezaji Ellie Mpanzu bado ana mkataba na Simba SC ambao hajaanza kuutumikia na ule wa awali haujaisha hivyo hawezi kugoma kwa kudai stahiki zake.

Tetesi zimekuwa zikieleza kuwa Mpanzu amegoma kucheza Simba SC mpaka alipwe stahiki zake za mkataba mpya wa miaka miwili aliyoongeza hivi karibuni.

Hakuwa kwenye kikosi cha Simba SC dhidi ya Coastal Union jambo ambalo liliongeza nguvu kwenye tetesi hizo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa hakuna ukweli kuhusu Mpanzu kudai stahiki zake za mkataba mpya.

“Mpanzu ana mkataba na Simba SC ambao unatarajiwa kuisha mwezi wa 8 hivyo bado ni mchezaji  wa Simba SC mpaka muda huu hakuna ambacho anakidadi kwa mkataba wake mpya ambao bado haujaanza kutumika.

“Ni ajabu mfanyakazi kuanza kudai stahiki zake za mkataba mpya ambao bado hajaanza kuutumikia ilihali ana mkataba na haujaisha hivyo haiwezekani kwa namna yoyote ile. Hayo mengine ni maneno tu kwa kuwa mkataba ulioongezwa bado haujaaanza kutumika,”.

Simba SC inatarajiwa kucheza na Azam FC kesho Aprili 5, 2026 Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba SC 0-2 Azam FC.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.