Mbeya City wapindua meza mbele ya KMC FC

MBEYA City hawataki utani baada ya kupindua meza kibabe mbele ya KMC FC katika mchezo wa NBC Premier League, Aprili 3, 2026, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Licha ya KMC FC kuanza kufunga magoli kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa walikwama kulinda ushindi huo na mwisho ubao ukasoma Mbeya City 3-2 KMC FC wakipishana na pointi tatu nyingine mazima.

Ni Oscar Paul alifungua ukurasa wa kufunga dakika ya 44 na Juma Shemvuni dakika ya 78 kwa KMC FC huku Mbeya City wakifunga kupitia Riphat Khamis dakika ya 64, Adili Buha dakika ya 76, (p) na Said Naushad dakika ya 86 likiwa ni goli la ushindi.

Ni Riphat Khamis alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo mara baada ya mchezo.

Matokeo hayo yanaifanya KMC FC kusalia na pointi 8 nafasi ya 16 huku Mbeya City ikifikisha jumla ya pointi 16 nafasi ya 12.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.