Simba SC 2-0 Coastal Union NBC Premier League ilikuwa balaa

Simba SC 2-0 Coastal Union NBC Premier League ilikuwa balaa ndani ya dakika 90 baada ya magoli ya ushindi kufungwa dakika 45 za mwanzo.

Katika kipindi cha kwanza Coastal Union waliongeza nguvu kubwa kwenye ulinzi huku mlinda mlango, Chuma Ramadhani akiwa kikwazo namba moja kwa wenyeji kupata magoli kutokana na majribio yaliyokuwa yakifanywa kupitia kwa Gueye, Oura na Clatous Chama.

Iliwachukua Simba SC dakika 25 kuandika goli la kwanza kupitia kwa Seleman Mwalimu akitumia pasi ya kiungo Clatous Chama kwenye mchezo huo.

Zikiwa zinahesabiwa sekunde mchezo kwenda mapumziko, Simba SC ilipata goli dakika ya 45+2 kupitia kwa Ismail Traore na hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kiungo Shiza Kichuya wa Coastal Union alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo licha ya kuwa kwenye ubora dakika 67 zilitosha kwake nafasi yake ilichukuliwa na Ali.

Mchezaji Neo Maema alichaguliwa kuwa mchezaji bora na dakika ya 90 alionyeshwa kadi ya njano wakati ikisubiriwa filimbi ya mwamuzi kukamilisha mchezo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC kufikisha pointi 34 kwenye msimamo baada ya mechi 15 wanaishusha Azam FC iliyokuwa nafasi ya pili.

Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi 32 baada ya mechi 16. Mchezo ujao watakutana wababe hawa wawili Uwanja wa Azam Complex, Aprili 5, 2026 kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.