Kule Hispania Laliga inaizizi kunoga huku mafahari wawili FC Barcelona na Real Madrid wakikimbizana kwenye mbio za ubingwa. Je vipi nafasi ya Atletico Madrid?. Jisajili na Meridianbet na usuke jamvi hapa.
Katika ulimwengu wa soka la kisasa linalotawaliwa na kasi, ubunifu na umiliki wa mpira, kuna timu chache zinazojaribu kwenda kinyume na mkondo huo na mojawapo ni Atlético Madrid.
Atletico imekuwa timu iliyojijengea jina kwa nidhamu kali, moyo wa kupambana, na uwezo wa kushinda hata inapobanwa. Chini ya Diego Simeone, Atletico wamekuwa wakijulikana kwa mfumo wa kujilinda kwanza kabla ya kushambulia. Mfumo huu uliwapa mafanikio makubwa, lakini sasa unaanza kuonekana kuwa na mipaka.
Kwenye Laliga Atletico hawako nafasi ya kwanza. Wamebaki kuwa wapinzani wagumu, lakini si wale wanaotawala ligi. Tatizo lao kubwa ni kukosa uthabiti wanaweza kushinda mechi ngumu, lakini wakapoteza pointi kirahisi kwenye mechi wanazotarajiwa kushinda. Hii inawafanya wabaki nyuma ya wapinzani wao wakuu.
Atletico Madrid wamekuwa wakipambana kubaki kwenye nafasi za juu ambapo hadi sasa wapo nafasi ya 4 baada ya kukusanya pointi zao 57 kwenye michezo 29 ambayo wamecheza na wakiwa nyuma kwa pointi 16 kwa kinara wa ligi.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Timu hiyo ina wachezaji wazuri sana ambao hufanya vyema kwenye mechi kubwa na safari hii imeongeza wachezaji kama Ademola Lookman ambaye ataenda kusaidiana na kina Solorth, Giuliano Simeone, Koke na wengine kibao.
Julian Alvarez ambaye pia alijiunga na timu hiyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho, lakini pia ni mchezaji ambaye anahitaji sana na baadhi ya timu kutoka Uingereza ikiwemo, Chelsea, Arsenal na zingine. Lakini mpaka sasa bado mustakabali wake hujajulikana.
Simeone na vijana wake kwenye mashindano ya Copa del Rey wamefanikiwa kufika hatua ya Fainali baada ya kumtoa Barcelona na watakipiga dhidi ya Real Sociedad April 18, hili ni Kombe ambalo wanalitaka kwa hali na mali kutokana na ushindano uliopo kwenye mashindano mengine. Je Atletico watabeba Kombe hili?. ODDS KUBWA izpo Meridianbet ingia na ubeti sasa.
Atletico Madrid kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya yaani UEFA Champions League, wameendelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa wapo hatua ya Robo Fainali na wamepangwa kucheza dhidi ya FC Barcelona hivyo badi Simeone ana kibarua kizito kabisa mbele ya vijana wa Hans Flick.
Hii inatarajiwa kuwa mechi ngumu kabisa lakini pia kama wakichanga karata zao vizuri wanaweza wakaibuka na ushindi kwani hii si mara ya kwanza kukutana hawa wawili. Je unadhani Barca watakubali kutolewa kwenye UEFA?. Bashiri hapa.
Kwa ujumla, Atletico Madrid ni timu ambayo bado ina uwezo wa kushindana katika mashindano yote, lakini imekosa ule uthabiti wa kuwa mabingwa. Ili kurejea kileleni, wanahitaji kuongeza ubunifu katika safu ya ushambuliaji, kupunguza utegemezi kwa mchezaji mmoja, na kubadilika kimfumo ili kuendana na mahitaji ya soka la kisasa. Bila kufanya hivyo, wataendelea kubaki kwenye kundi la timu bora lakini si mabingwa wanaotawala.