Singida Black Stars 1-2 Azam FC NBC Premier League

Singida Black Stars 1-2 Azam FC NBC Premier League matokeo rasmi ya mchezo wa leo Aprili Mosi, 2026, Singida.

 Kwa mara nyingine tena wenyeji wamepoteza alama tatu muhimu kutoka kwa timu ambazo zipo ndani ya 3 bora kwenye msimamo wa ligi.

Ilianza kupoteza mbele ya Yanga SC kwa kufungwa goli 3-0 kisha Simba SC kwa kufungwa goli 2-1.

 Azam FC walianza kufunga dakika ya 50 kupitia kwa Lusajo Mwaikenda na dakika 12 mbele wakapachika goli la pili kupitia kwa kiungo Feisal Salum dakika ya 63 ya mchezo.

Goli pekee la Singida Black Stars limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 kwa faida ya pigo la faulo iliyosababishwa na Sadio Kanoute katika harakati za kuokoa hatari.

Matokeo haya yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 32 baada ya mechi 16 ikiwashusha Simba SC nafasi ya pili.

Singida Black Stars inasalia nafasi ya 6 kwenye msimamo na pointi zake ni 25 baada ya mechi 16. Vinara ni Yanga SC wenye pointi 38.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.