Matokeo ya mechi zilizopita Azam FC

Matajiri wa Dar, Azam FC leo Aprili Mosi 2026 watakuwa kwenye shughuli kuwakabili Singida Black Stars mchezo wa ligi.

Ni saa 10:00 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa, Uwanja wa Airtel kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu.

Hapa tunakusogezea matokeo ya mechi 5 kwa Azam FC ndani ya Machi, 2026 NBC Premier League:-

Machi 2, 2026, Pamba Jiji FC 2-2 Azam FC
Machi 5, 2926, Tanzania Prisons 0-0 Azam FC
Machi 11,2026, Dodoma Jiji FC 0-3 Azam FC
Machi 15, 2026, Azam FC 0-0 Yanga SC
Machi 19,2026, Mashujaa FC 0-0 Azam FC

Ushindi kwa Azam FC ni mchezo mmoja na sare katika mechi 4. Timu hiyo ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo ikiwa na pointi 29, haijapoteza mchezo ndani ya ligi.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.