Mohamed Salah mwenye miaka 33 raia wa Misri inaelezwa kuwa amekataa bonasi ya kiasi cha Pauni Milioni 20 (zaidi ya Sh64 bilioni) ili kuondoka Liverpool.
Salah amefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake mwaka mmoja mapema, jambo litakaloifanya Liverpool kuokoa jumla ya Pauni Milioni 40.8 za mishahara na bonasi.
Salah ilibidi asubiri mpaka 2027 kutokana na mkataba wake kusalia mwaka mmoja huku ikielezwa kuwa hajawa kwenye mahusiano mazuri na kocha wa sasa Arne Slot.
Inaelezwa kuwa huenda akaenda Saudia kwa changamoto mpya atakakolipwa mshahara mnono
Rekodi zinaonyesha kuwa amecheza mechi 435 kafunga magoli 255 na pasi 122 akiwa na mataji mawili ya Premier, Champions League 1.