Mpanzu afurahia kubaki ndani ya Simba SC

ELLIE Mpanzu winga wa Simba SC, raia wa DR Congo amesema kuwa ni furaha kwake kusalia katika familia ya timu hiyo kwa muda mwingine tena.

Machi 23,2026 taarifa rasmi kutoka Simba SC ilieleza kuwa winga huyo mwenye pasi 5 za mabao msimu wa 2025/26 ndani ya NBC Premier League ameongeza kandarasi ya miaka miwili.

Awali ilikuwa inatajwa kuwa mabosi wa Yanga SC wanaiwinda saini ya nyota huyo ambaye mkataba wake ulikuwa unakaribia kufika mwisho.

Mpanzu kwenye mechi za hivi karibuni akianzia benchi ama kikosi cha kwanza amekuwa na mchango ndani ya Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker.

Katika mchezo dhidi ya Singida Black Stars alifunga goli la ushindi alipoanzia benchi na mwisho ubao wa Uwanja wa Airtel ulisoma Singida Black Stars 1-2 Simba SC.

Mpanzu amesema: “Ni furaha kwangu kuendelea kusalia ndani ya familia ya Simba SC nimefurahi na nina amini kwamba nitaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.