Maguire na Mainoo warejea England, Tuchel aacha nyota kadhaa wakubwa

Kocha wa Timu ya Taifa ya England, Thomas Tuchel ametangaza kikosi cha wachezaji 35 kwa ajili ya michezo ya Kalenda ya FIFA ya mwezi Machi 2026 huku nyota wa Manchester United, beki Harry Maguire na kiungo Kobbie Mainoo wakirejeshwa kikosini wakati beki wa Real Madrid, Trent Alexander-Arnold na beki WA Man United, Luke Shaw wakitemwa.

England inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Uruguay Machi 27 kabla ya kuvaana na Japan Machi 31 ambapo mechi hizo za mwisho kabla ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 zitachezwa katika dimba la Wembley.

MAKIPA: Dean Henderson (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), James Trafford (Man City), Aaron Ramsdale (Newcastle Utd), Jason Steele (Brighton)

MABEKI: Dan Burn (Newcastle), Marc Guehi (Man City), Lewis Hall (Newcastle), Ezri Konsa (Aston Villa), Tino Livramento (Newcastle), Harry Maguire (Man United), Nico O’Reilly (Man City), Jarell Quansah (Leverkusen), Djed Spence (Tottenham), John Stones (ManbCity), Fikayo Tomori (AC Milan)

VIUNGO: Elliot Anderson (Nottm Forest), Jude Bellingham (Real Madrid), James Garner (Everton), Jordan Henderson (Brentford), Kobbie Mainoo (Man United), Declan Rice (Arsenal), Morgan Rogers (Aston Villa), Adam Wharton (Crystal Palace)

WASHAMBULIAJI: Jarrod Bowen (West Ham), Dominic Calvert-Lewin (Leeds Utd), Eberechi Eze (Arsenal), Phil Foden (Man City), Anthony Gordon (Newcastle), Harry Kane (Bayern Munich), Noni Madueke (Arsenal), Cole Palmer (Chelsea), Marcus Rashford (Barcelona), Bukayo Saka (Arsenal), Dominic Solanke (Tottenham)