Simba SC vs TRA United fupa jingine gumu ndani ya NBC Premier League, Machi 22,2026, Uwanja wa Meja Isahmuyo.
Hiyo ni mara baada ya mchezo uliopita kwa mnyama kuangausha pointi mbili ugenini dhidi ya TP Lindanda, Mwanza.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kirumba ulisoma, Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC wakigawana pointi mojamoja.
Kituo kinachofuata kwa mnyama ni dhidi ya TRA United ikiwa ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba mchezo wa TRA United vs Simba SC uliotarajiwa kuchezwa Tabora uliahirishwa kutokana na eneo la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kujaa maji na mpira kushindwa kudunda hivyo utapangiwa tarehe nyingine.
Kwenye msimamo Simba SC ipo nafasi ya 3 imekusanya pointi 28 baada ya mechi 13 inakutana na TRA United SC nafasi ya 10 mechi 15 pointi 20.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.