Issa Mbuzi tambo zatawala kwa kuvuna pointi 3 za Mbeya City

ISSA Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate amebainisha kuwa wana timu bora ambayo inastahili ushindi kwenye mechi za ushindani ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.

Machi 3 2026 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine Mbeya ulisoma Mbeya City 0-1 Fountain Gate, goli la ushindi likifungwa na Said Ramadhan.

Mfungaji huyo wa goli la ushindi alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa na goli lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 71.

Mbuzi amesema: “Tuna timu bora yenye wachezaji wazuri na hata tulipofungwa na TRA United nilimwambia Christina Mwagala kuwa timu yao mbovu ila imetufunga.

“Hapa Mbeya tumecheza mchezo mzuri na kuvuna pointi tatu muhimu hii inatokana na ubora wa wachezaji na kujituma bila kuchoka,”.

Fountain Gate kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 15 huku Mbeya City ikiwa na pointi 13 nafasi ya 14 zote zimecheza mechi 15.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.