Klabu ya Misri, Al Ahly, imepewa pigo kubwa la kifedha baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuiamuru kulipa fidia ya dola za Kimarekani 588,000 (takribani Shilingi bilioni 1.53 za Kitanzania) kwa aliyekuwa kocha wake, José Riveiro.
Uamuzi huo umetolewa na Court of Arbitration for Sport (CAS) kufuatia mgogoro wa kisheria uliotokana na kusitishwa kwa mkataba wa Riveiro miezi mitatu tu baada ya kuteuliwa.
Kocha huyo alisaini kandarasi ya miaka miwili lakini alifutwa kazi mapema katika msimu wa 2025 kutokana na matokeo yasiyoridhisha. Hata hivyo, CAS imebaini kuwa kusitishwa kwa mkataba hakukufuata kikamilifu masharti ya fidia na haki za kimkataba alizostahili.