Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC rekodi mpya yaandikwa

Dodoma Jiji FC 0-0 Simba SC rekodi mpya yaandikwa mara baada ya mchezo kukamilika Februari 25,2026 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Rekodi hiyo ni kuwa mchezo wa kwanza kukamilika bila kupatikana goli ndani ya dakika 90 kwa wapinzani hawa wanapokutana.

Kwenye mechi 10 zilizopita wababe hawa walipokutana magoli yalikuwa yanafungwa na mchezo wa mwisho walipokutana ubao wa Uwanja wa KMC Complex Dar ulisoma Simba SC 6-0 Dodoma Jiji FC.

Rekodi nyingine mpya ambayo imeandikwa inakuwa ni mara ya kwanza kwa Dodoma Jiji FC kuvuna pointi mbele ya Simba SC.

Katika mechi 10 zilizopita wababe hawa walipokutana Simba SC ilikuwa ikipata ushindi hivyo mchezo wa 11 unakuwa ni sare na pointi moja ya kwanza inakwenda Dodoma Jiji FC na pointi moja kwa mnyama Simba SC.

Kituo kinachofuata kwa Simba SC ni Yanga SC vs Simba SC, Machi Mosi, 2026, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.