Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, kufuatia tukio la kuwahimiza wachezaji wake kutoka nje ya uwanja wakati wa mechi ya fainali ya AFCON 2025.
Tukio hilo lilitokea baada ya mwamuzi kuamua mkwaju wa penalti dakika za mwisho, ambayo ilionekana kuwa ya utata na kusababisha hisia tofauti miongoni mwa wachezaji na waofisa wa benchi la ufundi la timu ya Senegal, kwa kuonyesha kukatishwa tamaa na kutoridhishwa na uamuzi huo. Thiaw aliwaamuru wachezaji wake kuondoka uwanjani, hatua ambayo ilifanya mchezo kusitishwa kwa takriban dakika 15.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuwa kitendo hicho kimekiuka kanuni za mechi na heshima ya mashindano, hivyo kupelekea uamuzi wa kumsimamisha kocha huyo kwa muda usiojulikana.