Simba SC vs Mtibwa Sugar NBC Premier League

Simba vs Mtibwa Sugar ni mchezo wa NBC Premier League unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Januari 18,2026. Uwanja wa Mej.Gen. Isamuhyo.

Hii ni baada ya ligi kusimama kwa muda kutokana na mashindano ya AFCON ambayo yanaendelea nchini Morocco na Tanzania iliishia hatua ya 16 bora.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Jumapili, Januari 18,2026 itakuwa ni Senegal vs Morocco ambao ni wenyeji.

Kwa upande wa mchezo wa Simba SC vs Mtibwa Sugara unakuwa mchezo wa kwanza kwenye ligi ndani ya 2026 kwa wababe hawa wawili kukutana uwanjani.

Simba SC kwenye msimamo ni nafasi ya 5 ikiwa na pointi 12 baada ya mechi 5. Inakutana na Mtibwa Sugar nafasi ya 7 pointi 10 baada ya mechi 8. Vinara kwenye msimamo ni JKT Tanzania wakiwa na pointi 17 baada ya kucheza mechi 10.

Viingilio

Mzunguko ni 5,000
VIP ni 10,000

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.