Timu ya taifa ya Misri imetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi dhidi ya Benin kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa leo Januari 5 2026.
Mchezo huo umekwenda mpaka dakika ya 120 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja Adrar,Agadir kusoma Misri 1-1 Benin. Katika dakika 30 Misri ilifunga magoli mawili.
Misri walianza kufunga kipindi cha pili na Benini waliweka usawa zikiwa zimesalia dakika 7 kukamilika dakika 90 za mchezo.
Watupiaji kwa Misri ni Marwan Attia dakika ya 69, Yasser Ibrahim dakika ya 97 na Mo Salah dakika ya 120+4 goli la Mali limefungwa na Jodel Dossou dakika ya 83.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.