Meridianbet imeendelea kudhihirisha kuwa mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na kugusa maisha ya jamii kwa vitendo, baada ya kutembelea kituo cha watoto yatima cha Faraja Care Orphanage Centre kilichopo Mburahati. Kupitia ziara hiyo ya kijamii, kampuni hiyo ililenga kuleta tabasamu na matumaini mapya kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa masomo.
Katika tukio hilo, Meridiansport ilitoa msaada wa vifaa muhimu vya shule vikiwemo mabegi, madaftari, vitabu na kalamu, ili kuwawezesha watoto hao kuanza safari yao ya kielimu wakiwa na maandalizi kamili. Msaada huo umetolewa kwa lengo la kupunguza changamoto za kimahitaji ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya masomo ya watoto yatima.

Meridiansport inakupa taarifa mbalimbali za michezo ya kitaifa & kimataifa pamoja na uchambuzi wa michezo mbalimbali. Ingia leo kupitia meridiansport.co.tz na uanze kuburudika kwa taarifa mbalimbali za hapo kwa hapo ndani na nje ya nchi.
Akizungumza kwa niaba ya Meridiansport, mwakilishi wa kampuni hiyo Nancy Ingram alisema kuwa msaada huo unatokana na imani ya dhati kuwa kila mtoto anastahili fursa sawa ya kupata elimu bora na mazingira salama ya kukua. Alisisitiza kuwa Meridiansport itaendelea kushiriki katika shughuli za kijamii zinazolenga kuimarisha ustawi wa jamii na kuwawezesha makundi yenye uhitaji maalum.
Kwa upande wao, wanufaika wa msaada huo walionesha furaha na shukrani kubwa, wakieleza kuwa vifaa hivyo vitawapa hamasa mpya ya kuzingatia masomo yao bila hofu ya kukosa mahitaji ya msingi ya shule. Walezi wa kituo hicho pia walipongeza hatua ya Meridiansport, wakieleza kuwa imeleta matumaini mapya na imethibitisha kuwa bado kuna wadau wanaojali mustakabali wa watoto yatima.
Hatua hii ni sehemu ya mkakati mpana wa Meridiansport wa uwajibikaji kwa jamii, unaolenga kusaidia sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya na mazingira. Wakati ikiendelea kugusa maisha ya jamii, Meridiansportt pia inaendelea kuwa sehemu pekee ya kupata habari za michezo zilizoandaliwa kwa kina na zenye uhakika wakati wote.