MCHEZO wa hatua ya makundi AFCON 2025 ikiwa ni kundi C umekamilika nchini Morocco na ubao unasoma Nigeria 2-1 Tanzania.
Dakika 45 za mwanza Nigeria walipata goli la kuongoza na kipindi cha pili walipata goli la pili la ushindi lililowapa pointi tatu muhimu.
Ni Semi Ajay alifungua ukurasa wa magoli dakika ya 36 na Ademoola Lookman alipachika goli la pili dakika ya 52.
Kwa upande wa Tanzania ni Charlse M’mombwa dakika ya 50 ikiwa ni dakika 5 baada ya kurejea kutoka mapumziko na lilidumu kwa dakika mbili pekee.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.