Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) ‘The Leopards’ imeanza vyema kampeni yake ya AFCON 2025 baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Benin katika mchezo wa Kundi D.
Bao pekee la mchezo lilifungwa mapema dakika ya 16 na Theo Bongonda, akitumia vyema nafasi iliyopatikana na kuipa DR Congo pointi tatu muhimu kwenye mwanzo wa mashindano.
FT: DR Congo 🇨🇩 1-0 🇧🇯 Benin
⚽ 16’ Bongonda
Ushindi huu unaipa DR Congo mwanzo mzuri wa kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye hatua ya makundi, huku Benin wakilazimika kurekebisha makosa yao kabla ya mchezo unaofuata.