Mabingwa wa Dunia, Chelsea, wameonyesha ubabe mkubwa baada ya kuicharaza Barcelona mabao 3-0 katika dimba la Stamford Bridge, kwenye mchezo uliotawaliwa na wenyeji kwa muda mrefu.
Chelsea 3-0 Barcelona
⚽ 27’ Kounde (og)
⚽ 55’ Estêvão
⚽ 73’ Delap
🟥 44’ Araujo (Barcelona)
Barcelona walijikuta wakiwa pungufu muda mfupi kabla ya mapumziko baada ya Araujo kuonyeshwa kadi nyekundu, jambo lililofungua njia ya Chelsea kuongeza kasi na kumaliza mchezo wakiwa kifua mbele.
Man City wapigwa Etihad
Katika dimba la Etihad, wenyeji Manchester City walijikuta wakipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya vigogo wa Ujerumani, Bayer Leverkusen, katika mchezo ambao vijana wa Xabi Alonso walionekana imara zaidi kiufundi na kimkakati.
Manchester City 0-2 Bayer Leverkusen
⚽ 23’ Grimaldo
⚽ 53’ Schick
Matokeo Mengine ya Ulaya
Dortmund 4-0 Villarreal
Borussia Dortmund waliichapa Villarreal kwa jumla ya mabao 4-0, wakionyesha ubabe wao katika ardhi ya nyumbani.
Bodø/Glimt 2-3 Juventus
Juventus walipata ushindi muhimu ugenini licha ya upinzani mkali kutoka kwa Bodø/Glimt.
Marseille 2-1 Newcastle
Wakali wa Ufaransa, Marseille, waliwazidi nguvu Newcastle katika mchezo mkali uliochezwa Stade Vélodrome.
Napoli 2-0 Qarabağ
Napoli walitawala mchezo na kutwaa alama tatu muhimu nyumbani.
Slavia Praha 0-0 Athletic Club
Mchezo huu uliisha bila kufungana licha ya nafasi kadhaa za wazi kwa pande zote.
Ajax 0-2 Benfica
Ajax waliangukia nyumbani kwa mabao 2-0, Benfica wakionyesha nidhamu ya juu uwanjani.
Galatasaray 0-1 Union SG
Union SG waliandika ushindi mwembamba lakini muhimu ugenini nchini Uturuki.