Kuwait 4-3 Tanzania, sababu zakupoteza zatajwa

Ikiwa ni mchezo wa kwanza wa ushindani kwake Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars amesema kuwa kukosa umakini hasa kipindi cha pili ni sababu kubwa ya kupoteza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ga Kuwait.

Mchezo huo upo katika kalenda ya FIFA ulichezwa Novemba 15,2025 nchini Misri na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kuwait 4-3 Tanzania.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na M’Mombwa alitupia mawili dakika ya 6,87 na bao moja likifungwa na Allarakhia dakika ya 34. Katika dakika 45 za mwanzo Tanzania ilikamilisha ikiwa inaongoza kwa mabao mawili na mabao manne yote yalifungwa kipindi cha pili.

Mabao yalifungwa na Daham alitupia mawili dakika ya 46 na 52, Nasser dakika ya 63 na Hamdan dakika ya 69 kwa upande wa Kuwait.

Gamondi amesema: “Tulikuwa na mwanzo mzuri hasa kipindi cha kwanza lakini tukikosa umakini kipindi cha pili. Ninaweza kusema kuwa bao la pili tulifungwa kutokana na makosa yetu na mengine tulifungwa kwa mipira ya adhabu hivyo kuna sehemu tumeona inabidi kufanyia kazi zaidi.

“Nilifurahishwa na wachezaji namna walivyojitoa kipindi cha kwanza tulikuwa na umiliki wa mpira mzuri na umakini lakini kipindi cha pili kuna vitu vilipungua hivyo tutafanyia kazi kwa mechi zijazo,”.

Kikosi kazi cha kwanza cha Gamondi kilikuwa namba hii:-

Yakoub Suleman, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen, Dickson Job, Bakari Nondo, Alphonce Mabula, Novatus Dismas, Abdul Suleman, Charles M’Mombwa, Kelvin John na Tarryn Allakhia.

Wachezaji wa akiba walikuwa ni Hussen Masalanga, Zuber Foba, Pascal Msindo, Wilson Nangu, Idd Nado, Kelvin Nashon, Khalid Habibu, Morice Abraham, Seleman Mwalimu na Paul Peter.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.