YANGA SC hesabu zao kimataifa

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kuona wanapata matokeo mazuri kwenye mechi zao mbili za kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz kwa sasa ipo kwenye maandalizi kuelekea kwenye mchezo ujao wa hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika.

Itakuwa dhidi ya Silver Striker ya Malawi mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 2025 Yanga SC wakiwa ugenini.

Kamwe amesema kuwa wanatambua mchezo ujao ni mgumu wanafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo mazuri hivyo mashabiki watambue kwamba mipango inaendelea na wao wanajukumu lakwenda kuishangilia timu.

“Safari inazidi kukolea kuna magari zaidi ya 20 ambayo yamekamilika. Mashabiki wanakwenda kwa wingi uhamiaji kwa ajili ya kupata hati za kusafira ikiwa ni kwa ajili ya kuelekea Mawili. Hili ni jambo zuri na linapaswa kuwa endelevu.

“Mchezo ujao ni mgumu na utakuwa na ushindani mkubwa tukianzia ugenini. Malawi kunaendeka kwa mashabii kutokana na utaratibu ambao upo hivyo wafanye mawasiliano kwa kuwa kila kitu kipo kwenye mpango mzuri,” amesema.

Yanga SC wanaendelea na kampeni ya Malawi Kunaendekea ambapo kila tawi linafanya mchakato kupata mashabiki watakaolekea Malawi. Miongoni mwa matawi hayo ni Tawi la Songwe, Tawi la Njombe Mjini, Tawi la Siga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.