ROMAIN Folz, Kocha Mkuu wa Yanga SC amekiongoza kikosi hicho kwenye mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa kimataifa, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga SC imetoka kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya Mbeya City uliochezwa Septemba 30 2025 wakatoshana nguvu kwa suluhu ya 0-0.
Baada ya mchezo huo tetesi zilkuwa zinaeleza kuwa huenda Folz akaondoka ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo wa timu hiyo kutokuwa mzuri.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi kuwa bado Romain ni Kocha Mkuu wa Yanga SC hivyo hakuna taarifa nyingine tofauti ambayo imetoka.
Oktoba 6 2025, Romain Folz amekiongoza kikosi cha Yanga SC kwenye mazoezi Uwanja wa KMC ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa hatua ya pili itakuwa dhidi ya Silver Strikers utakaochezwa Malawi Oktoba 18 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.