VINARA wa Ligi Kuu Bara Yanga leo watakuwa na kazi ya kutesti mitambo kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC.
Saa 10:00 jioni mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ikiwa ni kwa ajili ya hesabu za mchezo wao ujao dhidi ya Polisi Tanzania ambao ni wa ligi.
Januari 23 Yanga yenye pointi 32 itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zake kibindoni ni 18 inanolewa na mzawa Malale Hamsini.
Mbuni ni timu ambayo imetinga hatua ya 32 kwenye Kombe la Shirikisho na itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Lipuli FC ya Iringa.