UBAO wa Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kipindi cha pili unasoma Yanga SC 1-0 Simba SC ikiwa ni fainali ya Ngao ya Jamii 2025.
Kipindi cha kwanza dakika 45 zilikamilika kwa wababe hawa wawili kutoshana nguvu bila kufungana na kipindi cha pili mambo yalibadilika.
Ni Pacome alipachika bao la kuongoza kwa Yanga SC dakika ya 53 ukiwa ni mchezo ambao una ushindani mkubwa kwa pande zote mbili ndani ya uwanja.
Pacome alikamilisha kazi ambayo ilianzishwa na Maxi Nzengeli na jaribio hilo liliokolewa na Camara na Pacome alipokutana na mpira akiwa ndani ya 18 alifunga bao la kuongoza.
Mwamuzi Ahmed Arajiga kwenye mchezo wa leo amemuonyesha kadi ya njano Camara baada ya kufungwa bao hilo alionekana akilalamika jambo ambalo lilipelekea kuonyeshwa kadi ya njano.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.