SHOMARI Kapombe beki wa Simba SC amebainisha kuwa watajitoa kwa nguvu zote kuzuia makosa kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC ili wasifungwe.
Mchezo wa funga kazi msimu wa 2024/25 kwa wababe hawa wawili ulichezwa Juni 25 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC, mabao ya Pacome na Mzize yaliwapa pointi tatu Yanga SC.
Leo Septemba 16 2025 unakwenda kuchezwa mchezo wa kwanza ikiwa ni kufungua pazi la Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 inayotarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025 na mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz.
Yanga SC na Simba SC zinatarajiwa kukutana leo Uwanja wa Mkaka kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.
Kapombe amesema: “Tunatambua msimu uliopita tulifungwa na Yanga SC, hata ukiangalia safu yao ya ushambuliaji ilifunga mabao mengi kuelekea mchezo wetu ujao makosa tumefanyia kazi ili tupate matokeo mazuri.
“Kila mchezaji yupo tayari na benchi la ufundi limetupa mbinu ambazo zitatupa matokeo uwanjani, tupo tayari na mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.”
Tayari mwamuzi wa kati ametajwa kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa 11:00 jioni ambaye ni Ahmed Arajiga.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.