HAWA HAPA MAPILATO YANGA SC VS SIMBA SC, KAYOKO KWENYE ORODHA

JOTO la Kariakoo Dabi linazidi kupanda kwa kasi ambapo watani hawa wa jadi wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Mkapa, Septemba 16 2025 katika mchezo wa fainali.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Cliford Ndimbo ametaja orodha ya waamuzi ambao watakuwa kwenye mchezo huo muhimu wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.

Ikumbukwe kwamba waamuzi hao watakabidhiwa vifaa vya kazi kutoka JustFit ambao wamebainisha kuwa watatoa na mipira maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hawa hapa waamuzi wa  Kariakoo Dabi, Septemba 16 2025, Ngao ya Jamii namna hii:-Mwamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga, mwamuzi msaidizi ni Mohamed Mkono, mwamuzi msaidizi namba 2 ni Kassim Mpanga, mwamuzi wa akiba ni Ramadhani Kayoko na mtathimini waamuzi ni Soud Abdi.

Mchezo wa mwisho wababe hawa wawili kukutana ilikuwa ni Juni 25 2025 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC, hivyo hii ni kete ya kwanza kwa watani hawa wa jadi ndani ya uwanja.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.