KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Jean Ahoua bado yupo ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna timu zaidi ya mbili ambazo zinahitaji saini yake lakini hawajafikia makubaliano mazuri kwa sasa kutokana na mchezaji huyo kuwa na mkataba wa mwaka mmoja.
Timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini ya mfungaji huyo namba moja kwenye ligi namba nne kwa ubora ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na inaelezwa kuwa kuna timu nyingine kutoka Misiri inahitaji saini yake.
Ahoua aliyefunga mabao 16 na pasi 9 za mabao yupo kwenye orodha ya wachezaji wa Simba SC kilichokwea pipa kuelekea Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.
Mbali na Ahoua kuwa kwenye msafara wa Simba SC utakaoweka kambi nchini Misri yupo kiungo mshambuliaji Awesu Awesu, Steven Mukwala, Joshua Mutale.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.