Yanga SC 4-0 JKT Tanzania

Yanga SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliochezwa leo, Agosti 24, 2026, Uwanja wa KMC Complex,Mwenge, Dar.

Ni Albert Kangwanda alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 29,Ibrahim Bacca aliongeza bao la pili dakika ya 34, Chadrack Boka alifunga dakika ya 39.

Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika ubao ulikuwa unasoma Yanga SC 3-0 JKT Tanzania. Kipindi cha pili, Yanga SC iliendelea kutawala mchezo na juhudi zake zilizaa matunda dakika ya 64, ambapo mshambuliaji Peter Shalulile alipata asisti kutoka kwa Albert Kangwanda akafunga bao la 4.

Nyota Kangwanda alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, alifunga bao moja na kutoa pasi mbili akihusika kwenye mabao matatu katika mchezo wa leo wakiwa nyumbani.

Huu ni ushindi wa tatu wakifikisha jumla ya mabao 11 na kuruhusu mabao mawili pekee. Yanga SC inawashusha watani zao wa jadi Simba SC kileleni wakiwa na pointi 9, tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Duniani kote kinapatikana mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.