FIFA Club World Cup 2025 mashindano haya yalianza kurindima Juni 14 na kugota mwisho Julai 13 2025 ambapo ni Chelsea kutoka England ilitwaa taji hilo mbele ya PSG kwa ushindi wa mabao 3-0 ni usiku wa kuamkia Juni 14 fainali ilichezwa.
Ni mabao ya Cole Palmer ambaye alifunga mabao mawili dakika 22 na 30 mbele ya PSG na bao moja likifungwa na Joao Pedro dakika 43. Kazi iliisha kabla ya mapumziko mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump ambaye alikuwa sambamba na Rais wa FIFA Gianni Infantino.
Enzo Maresca aliwapa mbinu wachezaji wa Chelsea kupata ushindi mbele ya PSG. Mashabiki wengi hawakutarajia hili ila imetokea. Mbinu za Luis Enrigue Kocha Mkuu wa PSG zilikwama.
Luis Enrique alipata makasiriko baada ya kupoteza mchezo huo. Ilionekana walikuwa kwenye mzozo na Joan Pedro wa Chelsea.
Kulikuwa na makundi 8 katika mashindano na viwanja 12 vilitumika kwa ajili ya mechi 63 ambazo zilichezwa nchini Marekani ambao walikuwa wenyeji wa mashindano haya makubwa.
Fainali ilichezwa Uwanja wa MetLife na mchezo wa ufunguzi ulichezwa Uwanja wa Miami’s Hard Rock.
Taji la FIFA Club World Cup ambalo ni jipya ubunifu wake umepita kwa wataalamu kutoka FIFA wakishirikiana na Global Luxury Jeweller Tiffany & CO.
Shughuli za ushindani ilikuwa ni kutoka timu 32 ambazo zilishiriki mashindano hayo makubwa na Bara la Afrika pia kulikuwa na timu ambazo zilishiriki.
Afrika ni timu nne ambapo tatu zilipatikana kutoka CAF Champions League na moja kutokana na raking yao, Asia timu 4, Europe 12, America ya Kati timu 4, Oceania timu moja, America ya Kusini timu 6 na timu mwenyeji alitoa timu moja.
Source: FIFA, MailOnline
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka na Mtandao. Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.