JUNI 25 2025 ni Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mzunguko wa pili msimu wa 2024/25. Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 79 wanakutana na Simba SC nafasi ya pili na pointi 78.
Kwenye eneo la viungo kuna vita kubwa ya namba kwa wachezaji. Ipo hivyo katika eneo la ulinzi ambapo kipa Djigui Diarra vita yake kubwa ni dhidi ya Mousa Camara wa Simba SC.
Kwa viungo washambuliaji, Pacome Zouzoua ndani ya Yanga SC iliyofunga mabao 81 amehusika katika mabao 20. Amefunga mabao 11 na kutoa pasi 9 za mabao. Ni dakika 1,536 kayeyusha. Kacheza jumla ya mechi 25 kati ya 29 ambazo Yanga SC imecheza.
Kwenye mabao 11 ambayo amefunga kafunga bao moja kwa penalti ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex mlinda mlango wa Kagera Sugar alikuwa ni Ramadhani Chalamanda.
Simba SC ni Jean Ahoua amehusika katika mabao 25.
Simba SC imefunga jumla ya mabao 69. Ni pasi 9 kateneneza akifunga mabao 16. Ni kinara katika chati ya wafungaji kwa sasa. Mzawa anayepambania kwa ukaribu ni Clement Mzize wa Yanga SC mwenye mabao 13.
Ahoua amecheza jumla ya mechi 27 kati ya 29 akikosekana katika mechi mbili ambazo ni dakika 180. Katika mabao 16 aliyofunga kafunga mabao 6 kwa penalti. Penalti yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji.
Kwa upande wa makipa Camara anaongoza kwa hati safi akiwa nazo 19 kibindoni. Camara ni mechi 27 amekaa langoni akifungwa mabao 11. Mechi mbili ni Ally Salim alikaa langoni na hakufungwa. Amekomba dakika 2,430 Camara.
Diarra ni mechi 22 alikaa langoni dakika 1,980 hati safi ni 16 akifungwa mabao 8. Juni 22 2025 hakuwa langoni dhidi ya Dodoma Jiji, Aboutwalib Mshery alikaa langoni. Baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.