YANGA SC vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, kituo kinachofuata ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa, Juni 25 2025 kwa wababe hao kukutana kusaka pointi tatu muhimu.
Mchezo uliopita kwa Yanga SC, raundi ya 30 Juni 22 2025 ubao wa Uwanja wa New Amaan ulisoma Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji. Katika mchezo huo bao la ufunguzi lilifungwa na Clatous Chama dakika ya nne akitumia pasi ya Clement Mzize.
Yanga SC ni timu namba moja kweny msimamo wa ligi ikiwa na pointi 79 inakwenda kukutana na timu namba mbili ambayo ni Simba SC ikiwa na pointi 78 zote zimecheza mechi 29 ndani ya ligi.
Pacome Zouzoua ni miongoni mwa viungo waliohusika kwenye mabao mengi katika kikosi cha Yanga SC akiwa kahusika kwenye mabao 20 kati ya 81 ambayo yamefungwa na Yanga SC.
Ni mabao 11 kafunga, alifunga mabao mawili mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine na katika mchezo huo Juni 18, Clatous Chama alipachika bao moja dakika ya 35 akitokea benchi.
Simba SC mkali wa mabao ni Jean Ahoua ambaye kafunga mabao 16 na pasi 9 akihusika kwenye mabao 25 kati ya mabao 69 yaliyofungwa na timu hiyo namba mbili kufunga mabao mengi ndani ya ligi.
Ahoua alianza katika kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Juni 22 2025 hakukomba dakika zote 90.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.