HAYA HAPA MATOKEO YA RAUNDI YA 30, MWISHO WA RELI KIGOMA KUGUMU

MZUNGUKO wa 30 umegota mwisho huku yakikusanywa mabao 26 uwanjani ni Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma pekee ngoma ilikuwa ngumu kwa wababe hao kushuhudia bao kwa upande wowote ule ikiwa ni funga kazi ndani ya msimu wa 2024/25.

Katika raundi ya 29 ni mabao 22 yalifungwa hivyo kasi imeongezeka raundi ya 30 yakiongezeka mabao manne ndani ya ligi.

Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji

Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji mabao yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 4, Duke Abuya dakika ya 50, Ibrahim Bacca dakika ya 62 ,Joash Onyango alijifunga dakika ya 90+4 na Maxi Nzengeli alikamilisha kamba ya tano dakika ya 90+7.

Simba SC 1-0 Kagera Sugar

Simba SC ilikomba pointi tatu kwa ushindi mbele ya Kagera Sugar. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC ulisoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar, bao la ushindi lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 17.

Fountain Gate 2-3 Azam FC

 Fountain Gate 2-3 Azam FC ni Mokono alipachika bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati, Kidemile alipachika bao la pili kwa Fountain Gate. Mabao ya Azam FC yalifungwa na Zidane dakika ya 3, Shiga alijifunga dakika ya 23 na bao la ushindi lilifungwa na Sopu dakika ya 90+2 kwa mkwaju wa penati.

Namungo FC 5-0 KenGold

 Namungo FC 5-0 KenGold mabao yalifungwa na Medie Kagere dakika ya 07 na 29, Hassan Kabunda dakika ya 41, Erasto Nyoni dakika ya 45,  Saleh Karabaka dakika ya 90+1.

Singida Black Stars 3-3 Tanzania Prisons

Singida BS 3-3 Tanzania Prisons, mabao ya Pokou 43, Tchakei dakika ya 45 na Jonathan Sowah dakika ya 47.Mabao ya Tanzania Prisons yalifungwa na Ismail dakika ya 63 mkwaju wa penati na dakika ya, 76 kwa penati, Haruna Chanongo dakika ya 84.

Pamba Jiji 1-1 KMC FC

Pamba Jiji 1-1 KMC FC ni Mathew Tegis alifunga kwa Pamba Jiji dakika ya 34  na Redemtus Musa alifunga kwa KMC.

Coastal Union 1-1 Tabora United

Coastal Union 1-1 Tabora United ni Lukas Kikoti alifunga dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati na Mwanengo alipachika bao kwa Tabora United dakika ya 53.

Mashujaa 0-0 JKT Tanzania

Mashujaa 0-0 JKT Tanzania ni mchezo pekee ambao ulikamilika bila wababe hawa kushuhudia bao ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.