ABDUL Sopu nyota wa Azam FC anayevaa uzi namba 9 utambulisho wake akiwa uwanjani amezidi kurejea katika ubora katika mechi za mzunguko wa pili baada ya kuwa nje kwa muda katika mzunguko wa kwanza.
Wakati Azam FC ikivuna pointi tatu mbele ya Tabora United Juni 18 2025, ubao wa Uwanja wa Azam Complex uliposoma Azam FC 5-0 Tabora United alihusika katika mabao mawili.
Sopu alifunga bao moja dakika ya 11 alipofungua pazia la mabao katika mchezo huo akitumia pasi ya Pascal Msindo likiwa ni bao lake la pili ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Ikumbukwe kwamba Mei 13 2025, baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 5-0 Dodoma Jiji, Sopu alifungua ukurasa wa mabao kwa kufunga bao moja na alitoa pasi moja alimpa Lusajo Mwaikenda ilikuwa dakika ya 5.
Mabao mengine ya Azam FC kwenye mchezo dhidi ya Tabora United yalifungwa na Gibril Sillah ambaye alifunga mabao mawili dakika ya 16 na dakika ya 29 akifikisha mabao 11 na pasi zake ni mbili.
Idd Nado alipachika bao moja dakika ya 45 na alitoa pasi moja kwa Sillah dakika ya 29 naye alihusika katika mabao mawili mfungaji wa kwanza ndani ya Azam FC kwenye mechi za ligi alipofungua ukurasa huo mbele ya KMC Complex,
Nassoro Saadun alipachika bao moja dakika ya 89 akitumia pasi ua Sopu anafikisha mabao 8 na pasi nne za mabao ndani ya Azam FC, msimu wa 2024/25.
Ndani ya dakika 180 kwenye mechi ambazo zimechezwa ndani ya Azam Complex ikiwa ni ile ya mzunguko wa 28 na 29, Azam FC imefunga jumla ya mabao 10 kwa kutembeza mwendo wa 5G.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.