KWENYE eneo la kuitafuta tuzo ya ufungaji bora kazi inazidi kupamba moto ndani ya ligi ambapo wachezaji wamekuwa wakifanya kazi kubwa kutimiza majukumu yao wakipambania kusepa na pointi tatu.
Katika eneo la utupiaji mabao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ni Jean Ahoua wa Simba SC ambaye ametupia jumla ya mabao 16 msimu wa 2024/25 akiwa ni namba moja.
Ahoua ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids amekuwa na zali kwenye namba ambapo anaongoza katika orodha ya wachezaji waliohusika katika mabao mengi.
Mbali na kufunga Ahoua ametengeneza pasi 8 za mabao ambazo zinamfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 24 kati ya 68 yaliyofungwa na Simba SC.
Mchezo ujao wa Simba SC ni dhidi ya Kagera Sugar unatarajiwa kuchezwa Juni 22 2025 ukiwa ni mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza Simba SC kuvuna pointi tatu ugenini kwa ushindi wa mabao 5-2.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Ahoua alifunga bao kwa pigo huru ikiwa ni bao lake la kwanza kufunga kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 na alifunga pia kwenye mchezo dhidi ya Pamba hivyo ni mabao mawili kafunga akiwa nje ya 18 kupitia pigo la faulo, free kick.
Juni 25 2025 itakuwa ni Yanga SC ambayo ina Clement Mzize na Prince Dube kwenye eneo la ushambuliaji wakiwa wote wametupia mabao 13 kila mmoja.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.