JUNI 15 2025 kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara mchezo namba 184 kati ya Yanga SC vs Simba SC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Simba SC wameruhusiwa kufanya mazoezi ya maandalizi Uwanja wa Mkapa na Wizara ya Michezo ila kuna hatihati mchezo huo ukapangiwa tarehe nyingine.
Licha yakuruhusiwa kufanya mazoezi ya mwisho Juni 14 Jumamosi, Uwanja wa Mkapa bado wenyeji wa mchezo Yanga SC wameshikilia msimamo wao kuwa hawatacheza mchezo namba 184 ambao ni mzunguko wa pili.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC Juni 9 2025 wakibainisha kuwa hawatacheza mpaka matakwa yao manne yakamilike hivyo hawajafanya maandalizi yoyote. Taarifa kutoka TPLB kwa sasa inasubiriwa kuamua hatma ya Kariakoo Dabi.
Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 73 Simba SC nafasi ya pili wakiwa na pointi 72 hivyo mchezo wa Kariakoo Dabi utatoa picha ya nani atakuwa kwenye nafasi nzuri kutwaa ubingwa wa ligi.
Mechi mbili za raundi ya 29 na 30 zote zimepangwa kuchezwa saa 10:00 kwa wababe wote kushuka uwanjani kukamilisha mzunguko wa pili.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.