MUTALE AWAGAWA MABOSI SIMBA SC

JOSHUA Mutale kiungo mshambuliaji wa Simba SC amewagawanya mabosi wa timu hiyo kutokana na wengine kuhitaji kuona anaondoka huku wengine wakihitaji kuona anabaki ndani ya kikosi hicho.

Mutale hakuwa kwenye mwanzo mzuri msimu wa 2024/25 kutokana na mechi ambazo alipewa nafasi kucheza chini ya kiwango.

Katika mechi za mzunguko wa pili Mutale amekuwa akifanya kazi kubwa pale anapopewa nafasi katika mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Ni yeye alifunga bao pekee kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane walipopoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 na kugotea nafasi ya pili.

Taarifa zinaeleza kuwa kumekuwa na mvutano wa mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakivutana kwa kuwa wapo wanaodhani hataendeleza ubora na wengine wakiamini kwamba bado ana uwezo wakuendelea kuwa kwenye ubora kwa msimu ujao.

Ni benchi la ufundi ripoti yao itaamua kwamba Mutale abaki ndani ya kikosi ama asepe kwa ajili ya kupata changamoto mpya sehemu nyingine kwa mkopo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.