SIMBA:TUNALITAKA KOMBE LA MAPINDUZI

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba ameweka wazi kwamba wanahitaji kutwaa Kombe la Mapinduzi hivyo watapambana ili kufikia malengo hayo.

Leo Januari 13, Uwanja wa Amaan, saa 2:15 inatarajiwa kuchezwa fainali kati ya Azam FC V Simba na mshindi wa mchezo huo atasepa na Kombe la Mapinudiz kwa mwaka 2022.

Barbara amesema kuwa wanatambua ubora na uimara wa Azam FC hawatawabeza kwenye mchezo wa fainali lakini malengo yao yapo palepale kuweza kutwaa Kombe la Mapinduzi.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu na Azam FC ni timu bora hilo tunalitambua, hakuna namna tutafanya vizuri na tunahitaji kutwaa Kombe la Mapinduzi.

“Kikubwa ni suala la kusubiri kwa sababu fainali inachezwa Alhamisi na kila timu inahitaji ushindi sisi tulishasema kwamba tunahitaji kutwaa Kombe la Mapinduzi,” amesema.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi walikuwa ni Yanga na waliondolewa na Azam FC kwenye hatua ya nusu fainali kwa changamoto ya penalti.

Azam FC ilishinda penalti 9-8 zilifungwa na Yanga na Yassin Mustapha alikuwa nyota pekee aliyekosa penalti kwenye mchezo huo huku Mudhathir Yahya yeye akifunga kwa upande wa Azam FC ile penalti ya mwisho.