HUYU HAPA ALIMJAZA NKANE KUHUSU KUCHEZA MUUNGANO CUP

KIUNGO wa Yanga, Dennis Nkane ameweka wazi kuwa aliambiwa na kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli kwamba atapata nafasi kwenye mechi za Muungano Cup, Zanzibar.

Nkane ndani ya Yanga kwenye mechi za ushindani hajawa na nafasi ya kwanza kikosi cha kwanza ambapo Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 70 baada yakucheza mechi 26.

Alipata nafasi yakucheza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya KVZ FC kwenye Muungano Cup akitokea benchi na Yanga ikpata ushindi wa mabao 2-0 na kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na Zimamoto FC, Aprili 29 2025.

Kiungo huyo amesema kuwa furaha kubwa kupata nafasi kwenye mechi za ushindani na aliamini kwamba kwa namna yoyote angefunga kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe ulivyokuwa.

“Maxi aliniambia kwamba kwa muda mrefu sijapata nafasi yakufanya jambo ndio maana nilipofunga alishangilia kwa furaha, ninanajua wachezaji wengi walifurahi lakini Maxi alifurahi zaidi.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu wenye ushindani mkubwa, niliwaambia wachezaji wenzangu ambao tulikuwa benchi kwamba nikiingia halafu nikafunga basi washangilie kwa nguvu kuwa sisi ni familia.

“Nilipofunga niliangalia wapo ambao hawakushangilia kwa nguvu najua hao nitaonana nao mwenyewe kwa kuwa mchezo huu tulikuwa tunauhitaji, kazi yetu ni kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki.”

Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 ambapo bao la ufunguzi lilifungwa na kiungo Aziz Ki na bao la pili alifunga Nkane ambaye alikuwa na nafasi yakutoa pasi kwa Aziz Ki aliyekuwa kwenye nafasi yakufunga bao hilo.

Yanga imetinga hatua ya nusu fainali itakwenda kumenyana na Zimamoto hatua ya nusu fainali na mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 29 2025 na mshindi wa mchezo wa Aprili 28 kati ya JKU ama Azam FC watakutana na mshindi wa nusu fainali ya Aprili 29.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.