Ikiwa ni Jumamosi ya wewe ndugu mteja kuondoka na kitita cha pesa pale Meridianbet, kampuni hiyo yenyewe leo hii imefika mpaka kata ya Mbezi Juu na kutoa msaada wa vifaa vya usafi.
Mapema kabisa timu nzima ya Meridianbet ikiongozwa na Nancy Ingram ambaye ni Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo, walifika katika Ofisi ya Diwani wa Mbezi Juu na kugawa vifaa vya usafi ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuimarisha usafi katika jamii.
Vifaa ambavyo vimeweza kugawiwa ni pamoja na Dustbins(mapipa ya usafi), glovu za usafi, Reflectors kwa viongozi wa mtaa, maafisa usafi pamoja na wawakilishi wa wananchi ambaye alikuwepo hapo.
Jumamosi ya leo chukua mzigo wako mapema ambapo mechi kibao zipo kwaajili yako siku ya leo. Suka jamvi lako la ushindi leo na ubashiri hapa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.
Ikumbukwe kuwa zoezi hilo la kukabidhi vifaa hivyo lilinoga zaidi baada ya uwepo wa viongozi mbalimbali akiwemo Diwani wa Kata ya Mbezi Juu, Mheshimiwa Anna Lukindo pamoja na wawakilishi kutoka Meridianbet.
“Meridianbet tunaamini kuwa usafi ni afya, na afya ni msingi wa maendeleo ya jamii. Kupitia zoezi hili, tunataka kutoa hamasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira yao. Tunatambua jukumu letu kama sehemu ya jamii, na hii ni hatua mojawapo ya kuonesha kuwa tunajali,” amesema Nancy Ingram.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mbezi Juu ameishukuru Meridianbet kwa moyo wa kizalendo na ushirikiano wao katika kuunga mkono juhudi za serikali za mitaa katika kuhakikisha mazingira yanabaki kuwa salama, safi, na yanayovutia.
“Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali katika kuhakikisha tunalinda afya na hadhi ya mazingira ya wananchi wetu. Tunatoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano huu,” amesema Mh. Anna Lukindo.
Vifaa vilivyotolewa vitasambazwa katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mbezi Juu ili kusaidia ukusanyaji bora wa taka, kulinda usalama wa watoa huduma za usafi, na kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika kutunza mazingira.
Meridianbet inasisitiza kuwa itaendelea kurejesha kwenye jamii, kwani bila jamii wao si kitu, hivyo pia wanawasihi watu wengine na kampuni zingine kuiga mfano kutoka kwao kwani wenye uhitaji ni wengi sana.