KOMBE LA MAPINDUZI RATIBA YA NUSU FAINALI

LEO Jumatatu, Januari 10,2022 inatarajiwa kuchezwa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar ambapo mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa.

Ni mabingwa watetezi wa taji hilo ambao ni Yanga wao watamenyana na Azam FC itakuwa ni saa 10:15 jioni.

Mchezo mwingine ni ule wa pili ambao utazikutanisha Simba v Namungo, itakuwa ni saa 2:15 usiku.

Washindi kwenye mechi hizi watakutana kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi ya Januari 13,2022.

Pia timu zote ambazo zinacheza leo ni zile zinazotoka Bara baada ya zile za Visiwani kuweza kuondolewa kwenye hatua ya makundi.