BAADA ya kukoseka kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara kiungo mkandaji wa Simba amerejea katika uwanja wa mazoezi ikiwa tayari kwa mechi zijazo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Kibu Dennis maarufu kwa jina la Mkandaji alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 0-3 Simba.
Ni mbele ya Fountain Gate walipotoshana kwa kufungana bao 1-1 na mchezo wa Tanzania Prisons wakati Simba ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa KMC, huku mtoto wa maajabu Ladack Chasambi akiwa ni mgeni rasmi na alianza kikosi cha kwanza.
Kibu ameanza mazoezi na wachezaji wenzake na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Namungo mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa.
Msim wa 2024/25 Kibu hajafunga bao ndani ya ligi lakini ni chaguo la kwanza la kocha Fadlu kutokana na uwezo alionao kwenye matumizi ya nguvu kupambana na mabeki wa kazi ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
Ikumbukwe kwamba wakati Simba ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars Kibu alikuwa miongoni mwa nyota walioanza kikosi cha kwanza na alikuwa akipambana na mabeki zaidi ya wawili wakiongozwa na Kenedy Juma ambaye ni nahodha wa Singida Black Stars.
Katika mchezo huo bao la Simba lilifungwa na Fabrince Ngoma ambaye alitumia pasi ya Jean Ahoua aliyepiga kona akiwa nje ya 18 na mwisho Simba wakasepa na pointi tatu mazima.
Anga la kimataifa, kwenye hatua za makundi Kibu Dennis ni namba moja kwa wakali wa kucheka na nyavu Simba akiwa ametupia mabao matatu kati ya mabao 8 ambayo timu hiyo imefunga ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi A.
Mchezo ujao kwa Simba dhidi ya Namungo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Februari 19 2025 kwa wababe hao kusaka pointi tatu muhimu.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.