HAPA NDIPO PATAKAPOWAANGUSHA SIMBA

ENEO la ushambuliaji litawaangusha Simba kwenye mbio za kuwania ubingwa ikiwa wachezaji watashindwa kuwa makini hasa katika umaliziaji wa nafasi na kutengeneza nafasi.

Katika michezo ambayo ameanza Mpanzu ameonekana kuwa na shauku kubwa yakutaka kufunga zaidi ya kutengeneza nafasi za mabao jambo linalowapa ugumu Simba kufunga ndani ya uwanja.

Nafasi ambazo wanazipata ndani ya 18 ni aghalabu kuzitumia zote kwa usahihi, kwa mfano mchezo dhidi ya Fountain Gate, Leonel Ateba alipata nafasi zaidi ya tano akatumia nafasi moja.

Mchezo dhidi ya KenGold, Joshua Mutale ndani ya 18 anashindwa kupiga shuti kulenga lango.

Mpanzu alikuwa na nafasi kutoa pasi zaidi ya pasi tatu zote akaamua kufunga mapigo yakawa ni hasara kwa timu.

Jean Ahoua akiwa ndani ya 18 anapiga shuti ambalo hata yeye mwenyewe anashangaa amepigaje nibkazi kubwa inahitajika eneo la kiungo na eneo la ushambuliaji kufanyiwa kazi bila kusahau back pass.

Chasambi hakuwa na siku nzuri tangu dakika ya mwanzo ndio maana mapigo yake matatu ya kona yote yalikuwa hovyo.

Bado Chasambi ana nafasi ya kurejea katika ubora na kuwa imara zaidi licha ya kujifunga kwenye mchezo wa ligi mbele ya Fountain Gate wakigawana pointi mojamoja ndani ya dakika 90.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo ule uliochezwa Februari 6 2025 ni yeye alitoa pasi ya bao kwa Ateba ambaye alifikisha jumla ya mabao 8 ndani ya ligi ni yeye alirudisha pasi yenye ujazo mkubwa kwa kipa Moussa Camara ambaye alikwama kuipata pasi hiyo mwisho ikawa bao la usawa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.