PEP GUARDIOLA NA MKEWE WAACHANA BAADA YA KUDUMU KWA MIAKA 30

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola na mkewe, Cristina Serra wameachana baada ya kudumu kwenye mapenzi kwa muda wa miaka 30.

Taarifa za ndoa yao kuvunjika, zimetolewa na Kituo cha Habari cha Sport cha nchini Hispania ambapo imeelezwa kuwa wawili hao wamekuwa wakiishi mbalimbali kwa takribani miaka mitano sasa, Guardiola akiishi Manchester, Uingereza na mtoto wao mmoja na Cristina akiishi Barcelona, Hispania na watoto wao wawili.

Penzi la wawili hao lilianza mwaka 1994 walipokutana, ambapo wamefanikiwa kupata watoto watatu, Maria (24) na Marius (22) na Valentina (17).

Sport imeripoti kuwa wawili hao walifikia uamuzi wa kuachana Desemba, 2024 ambapo ni watu wao wa karibu pekee ndiyo waliokuwa wakijua kuhusu mpango huo.